Powered By Blogger

Friday, 28 September 2012

KDF YATEKA KISMAYU



KDF yateka Kismayu

Jeshi la Kenya kwa ushirikiano na jeshi la Somalia SNA limefanikiwa kuuteka mji wa Kisimayu ambao ulikuwa ngome kuu ya Al Shabaab.

Msemaji wa oparesheni hiyo Kanali Cyrus Oguna amefichua kuwa wanajeshi hao waliuteka mji huo mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia leo. Ni juzi tu ambapo duru ziliarifu kuwa kundi la wanamgabo wa kiislamu Hizbul lilijitenga na kundi la Al Shabaab na hivyo kupunguza makali ya kundi hilo. Kutekwa kwa Kisimayu kunajiri siku kadhaa baada ya miji mingine kutekwa ikiwemo Ras Kamboni na Afamdhow ambayo ilikuwa makaazi ya wanamgambo hao. Jeshi la Kenya KDF liliingia nchini Somalia mwezi Oktoba mwaka jana kukabiliana na kundi hilo na kufanikiwa kuwaua mamia ya wafuasi hao. Baada ya Kenya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kulishuhudiwa visa kadhaa vya mashambulizi ya kigaidi na kupelekea vifo vya zaidi ya watu 100.

No comments:

Post a Comment